Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Qatar imeripoti kwamba Marekani imetoa wito wa kusitisha mapigano na Iran.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar: Rais wa Marekani Donald Trump alipiga simu na kuzungumza na Emir wa Qatar Tamim bin Hamad Al Thani baada ya shambulio la kombora la Iran kwenye kambi ya Marekani "Al-Udeid" iliyopo ndani ya Mji wa Doha - Qatar. Ilikuwa ni Washington iliyoiomba Qatar kuwasiliana na Iran na ili kujua jinsi ilivyokuwa tayari kusitisha mapigano.
Kulingana na kauli ya Al-Thani, baada ya ombi la Marekani la kuiomba iwasiliane na Iran ili kuiomba kukubali kusitisha vita, Doha ilifanya mawasiliano muhimu na upande wa Iran, na hatimaye umepatikana muafaka wa makubaliano ya kusitisha mapigano.
Your Comment